Mafao ya FADEMO

Ulinzi wa kijamii unaokua pamoja na mchango wako

Huduma kwa mwanachama

Msaada kwenye hatua muhimu za maisha.

FADEMO inaunganisha michango ya wanachama na mafao ya muda mfupi na muda mrefu. Angalia huduma, ingia kwenye akaunti yako, kisha tuma ombi lenye nyaraka zinazohitajika.

Huduma za mafao
Mafao 12 kwa mwanachama na wategemezi
12Aina za mafao
Short + LongMuda mfupi na muda mrefu
OnlineMaombi na majibu ndani ya akaunti
Katalogi ya mafao

Chagua huduma unayotaka kufahamu

Kiasi na ustahiki hutegemea ada, muda wa uchangiaji, deni na ushahidi wa tukio.

Mafao ya Uzazi

Mafao ya Uzazi

Msaada kwa mwanachama mchangiaji hai baada ya kupata mtoto kwa mujibu wa masharti ya mfuko.

Hadi TZS 2,500,000
Mafao ya Kufunga Ndoa

Mafao ya Kufunga Ndoa

Msaada kwa mwanachama mchangiaji hai anayefunga ndoa akiwa hana deni la ada au tozo.

Hadi TZS 1,500,000
Mafao ya Ujenzi wa Nyumba

Mafao ya Ujenzi wa Nyumba

Mabati au fedha kulingana na kiwango cha ada na uthibitisho wa ujenzi.

Mabati 100 au hadi TZS 3,000,000
Mafao ya Gari la Ndoto

Mafao ya Gari la Ndoto

Msaada wa fedha wa kuongeza kwenye ununuzi wa gari la biashara au kazi.

Hadi TZS 3,000,000
Mafao ya Matibabu

Mafao ya Matibabu

Msaada wa matibabu kwa mwanachama mchangiaji hai aliyelazwa hospitali na kukidhi vigezo.

Hadi TZS 900,000
Mafao ya Uchunguzi wa Afya

Mafao ya Uchunguzi wa Afya

Msaada wa vipimo vya afya kwa mwanachama ili kusaidia kugundua magonjwa mapema.

Hadi TZS 500,000
Mafao ya Msaada wa Mazishi

Mafao ya Msaada wa Mazishi

Msaada unapofiwa na ndugu wa karibu waliotambuliwa kwenye kanuni za mfuko.

Hadi TZS 1,500,000
Mafao ya Kinga ya Majanga

Mafao ya Kinga ya Majanga

Kinga dhidi ya ajali kubwa, moto, mafuriko, uvamizi au janga jingine linalotambuliwa.

Hadi TZS 800,000
Mafao ya Uzeeni (Kiinua Mgongo)

Mafao ya Uzeeni (Kiinua Mgongo)

Kiinua mgongo kwa mwanachama aliyefikia umri na masharti ya kustaafu.

Michango yote x 150%
Pensheni ya Kila Mwezi Uzeeni

Pensheni ya Kila Mwezi Uzeeni

Pensheni ya kila mwezi kwa mwanachama aliyefikisha muda wa uchangiaji na umri wa kustaafu.

Hadi TZS 800,000 kwa mwezi
Mafao ya Mirathi kwa Wategemezi

Mafao ya Mirathi kwa Wategemezi

Kiinua mgongo na/au pensheni kwa warithi halali wa mwanachama aliyefariki.

Kiinua mgongo na/au pensheni
Mafao ya Kujitoa

Mafao ya Kujitoa

Msaada kwa mwanachama anayejitoa kwa sababu maalum baada ya kutimiza vigezo vya mfuko.

Michango + hadi 5% faida
Jinsi ya kuomba

Hatua nne rahisi

Ingia kwenye akaunti

Tumia akaunti yako ya mwanachama.

Chagua fao

Fungua Mafao Dashboard na chagua huduma.

Pakia nyaraka

Ambatisha nyaraka na ushahidi wa tukio.

Fuatilia jibu

Angalia status na majibu ndani ya dashboard.

Uko tayari kuomba fao?

Ingia kwenye akaunti yako au jisajili kuwa mwanachama.