Warning: Undefined array key "userID" in /home/u733561284/domains/fademo.co.tz/public_html/functions/database_functions.php on line 70
FADEMO COMPANY

KUUNGANISHWA MIFUKO YA PENSHENI-MAFAO YAMEBORESHWA


Tafiti nyingi zilizowahi kufanywa na taasisi nyingi nchini zilipendekeza mifuko ya pensheni iunganishwe kuwa mmoja au miwili tu. Zoezi hilo linasemekana kuwa lilisubiriwa kwa kipindi kirefu sana. Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Kuundwa kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa umma ujulikanao kwa kirefu chake, “Public Service Social Security Fund” kwa kifupi“PSSSF”,ni mabadiliko makubwa ya kihistoria nchini Tanzania yanayopaswa kuwekwa kwenye kumbukumbu za taifa hili. Ni mabadiliko ambayo wadau wote wa maswala ya Hifadhi ya Jamii nchini hawana budi kuyaenzi na kuyafafanua kwa umma wa Tanzania. Mabadiliko haya makubwa (great social security reform) yanafanya Tanzania Bara kubaki na Mifuko miwili tu ya Hifadhi ya Jamii ambayo sasa ni PSSSF na NSSF. Mfuko wa PSSSF utatoa mafao kwa watumishi wa sekta ya umma huku NSSF ukitoa mafao kwa sekta binafsi. Ndani ya Kitabu hiki utapata ufafanuzi wa kina kuhusu mabadiliko hayo makubwa katika sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini. Mambo mazuri na makubwa ambayo wanachama wa Mfuko Mpya wa PSSSF watayapata kwa mujibu wa sheria iliyounda mfuko huo yameelezwa kwa kirefu.

Details

ISBN ISBN 9789987979769
Author Venerando J Milinga
book_pdf KUUNGANISHWA MIFUKO YA PENSHENI-MAFAO YAMEBORESHWA -Edited June 2024.pdf
Price 10000
publisher_name Fademo Publishing Co
created_at 2024-06-18 12:04:47